KUPPET YAENDELEA KULEMAZA MASOMO

Mamia ya walimu wa shule za upili wameandamana kwa siku 8 hii leo na kulemaza shughuli za masomo kote nchini wakiitaka tume ya kuwaajiri walimu TSC itekeleze mtakaba wa maelewano baina yake na walimu.
Mjini Kisii, walimu hao wamejitokeza katikati yam ji kutoa malalamishi yao ikiwemo kuwaajiri walimu wa JSS, kuwapandisha vyeo walimu waliohitimu na shahada na kuboresha bima yao ya afya.
Aidha, wamemetaka afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia kung’atuka mamlakani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa