MAWAZIRI WA USALAMA WA SADC NA EAC WAKUTANA KUJADILI GHASIA DRC
Mawaziri wa Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaendelea na mkutano wa pili leo, wakijadili suluhisho la kudumu kwa ghasia zinazoendelea nchini DRC.
Hii inajiri baada ya juhudi zao za awali za kutatua mzozo huo kwa njia ya kijeshi kushindwa kuleta matokeo yanayotarajiwa. Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti, akisisitiza kuwa wananchi wa Congo wameathirika pakubwa na machafuko hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete