#Sports

OGAM ASEMA AKO TAYARI KUMENYANA NA KAKAMEGA HOMEBOYZ

Mchezaji wa Tusker FC Ryan-Wesley Ogam ametangaza kuwa tayari kumenyana na Kakamega Homeboyz katika mechi ya mwisho ya msimu huu wikendi hii, baada ya kupona jeraha la goti lililomweka nje kwa miezi mitatu.

Kabla ya kuumia, Ogam alikuwa katika hali nzuri, akifunga mabao 15 na kutoa asisti tatu katika mechi 13 pekee wakati wa mkondo wa kwanza wa msimu.

Akitafakari kuhusu kipindi cha kujiuguza, Ogam alielezea masikitiko yake akisema amekosa shabaha yake ya msimu.

Kukosekana kwa Ogam katika mechi 11 za mwisho za ligi kuliathiri sana safu ya ushambuliaji ya Tusker, kwani walishinda mara nne pekee, sare nne na kupoteza mara tatu katika kipindi hicho – mwendo ambao ulikata matumaini yao ya ubingwa.

Imetayrishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *