KUVUNJA BUNGE: KOOME ABUNI JOPO, 5

Jaji mkuu Martha Koome amebuni upya jopo la majaji 5 wa mahakama kuu kusikiliza kesi inayopinga ushauri wa mtangulizi wake David Maraga wa kumtaka Rais kuvunjilia mbali bunge la kitaifa.
Mnamo mwaka 2020, Maraga alimshauri Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kuvunja bunge baada ya bunge hilo kushindwa kubuni sheria inayohakikisha usawa wa kijinsia, ushauri ambao ulipingwa na walalamishi 10 tofauti.
Jopo hilo litaongozwa na jaji Jairus Ngaah, likijumuisha majaji Lawrence Mugambi, Patricia Nyaundi, Moses Otieno na Tabitha Wanyama, kesi hiyo ikitajwa mbele yao tarehe 24 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa