WALUKE AWAONYA WAKAZI DHIDI YA KUANDAMANA

Mbunge wa Sirisia John Waluke amekashifu vikali mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayodaiwa kufadhili maandamano yanaoendeshwa na vijana wa kizazi cha Gen z akihoji kuwa maandamano hayo yanalemaza maendeleo kando na kuvuruga amani.
Akihutubu kwenye hafla moja eneo la sirisia, Waluke amesema maandamano hayo yametekwa na wahuni wanayotumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu.
Wakati uo huo, Waluke ametoa wito kwa vijana kukomesha maandamano hayo, na kuongeza kuwa kutupiliwa mbali kwa msada wa fedha kutalemaza miradi kadhaa ya serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa