CHEPTEGET HAYUPO MBIONI

Bingwa mpya wa Olimpiki wa mbio za mita 10,000 Joshua Cheptegei hatatetea taji lake la mbio za mita 5,000 mjini Paris.
Cheptegei, ambaye alishinda medali ya fedha katika Michezo ya Tokyo, alisema kupitia anwani yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba alichukua uamuzi huo baada ya mazungumzo na wasimamizi wake.
Alibainisha kuwa alijivunia kushinda dhahabu ya Olimpiki katika mbio za 10,000m, akiongeza kuwa medali hiyo ya dhahabu ilikamilisha mkusanyiko wake, baada ya taji la dunia la vijana mbio za mita 10,000, ubingwa wa dunia mara tatu mbio za mita 10,000 na rekodi ya dunia ya mbio hizo.
Mchujo wa mbio za mita 5,000 umeratibiwa kesho, huku fainali ikitarajiwa kuwa siku ya Jumamosi.
Imetayarishwa na Nelson Andati