WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAPANGA KUANDAMANO KUPINGA MFUMO WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU

Wanafunzi wa vyuo vikuu humu nchini wanatarajiwa kushiriki maandamano hii leo kupinga mfumo mpya wa ufathili wa elimu ya juu.
Baada ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuwekwa katika kategoria tano tofauti wanafunzi hnao wanapendekeza mfumo wa awali kurejelewa.
Kufikia sasa wanafunzi zaidi ya 13000 wamewasilisha malalamishi yao wakipinga kuwekwa katika kategoria zisizowiana na mapato ya familia zao.
Mfumo huo umekosolewa pakubwa na sio tu wanafunzi bali pia baadhi ya viongozi wa azimio.
Imetayarishwa na Janice Marete