#Business

WATU ZAIDI YA MILIONI 74 WAKABILIWA NA UHABA WA CHAKULA BARANI AFRIKA

Ripoti ambayo imetolewa  na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD), imeonyesha kuwa takriban watu milioni 74.9 katika kanda ya Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Kufuatia ripoti hiyo kati ya idadi ya watu milioni 46.8 ni wananchi kutoka nchi saba kati ya wanachama wanane wa IGAD zikiwemo Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania, Sudan na Uganda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ripoti hiyo pia imenakili kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu wenye uhaba wa chakula katika ukanda wa afrika kutoka watu milioni 58.1 mwezi Februari mwaka huu wa 2024 hadi milioni 74 kumesababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa ambayo imeshuhudiwa sehemu mbali mbali.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *