KOCHA MKUU WA ULINZI STARLETS ANA MATUMAINI KWA KIKOSI CHAKE
Kocha mkuu wa Ulinzi Starlets, Collins Ochieng, ana matumaini kikosi chake kitatwaa Kombe la FKF kwa Wanawake kwa mara ya nne mfululizo.
Ulinzi waliunganishwa na TUK Ravens katika mechi yao ya ufunguzi wa toleo la 2025, baada ya droo kuandaliwa Jumanne katika hoteli moja Nairobi.
Timu zilizoshiriki katika droo hiyo zilitoka kwa vilabu vya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, mikoa na kaunti.
Wanajeshi hao walishinda toleo la 2024 baada ya kuifunga Kibera Soccer Ladies 2-1 katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Police Sacco Stadium Julai 10, shukrani kwa mabao ya Sheryl Angachi na Linda Kihara.
Raundi ya awali pia itawakutanisha Gaspo na Kibera Soccer Women, Barcelona Ladies wakichuana na Bungoma Queens, Thika Starlets wakimenyana na Kenya Police, huku Marine Queens wakicheza na Zetech Sparks.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































