LIVERPOOL WAKARIBIA KUTWAA TAJI LA EPL

Liverpool wako hatua chache kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza baada ya ushindi wa 2–1 dhidi ya West Ham, bao la ushindi likifungwa na Virgil van Dijk dakika za mwisho. Luis Diaz alifungua ukurasa kabla ya Andrew Robertson kujifunga, lakini Van Dijk akaamua matokeo kupitia kona ya Alexis Mac Allister.
Liverpool sasa wanaongoza kwa pointi 13 mbele ya Arsenal, na wanaweza kutawazwa mabingwa Aprili 20 iwapo Arsenal watapoteza dhidi ya Ipswich na wao washinde dhidi ya Leicester. Wakiwa na mechi sita tu zilizobaki na wakihitaji pointi sita pekee, Slot yuko karibu kufanikisha taji la 20 la klabu hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete