POLICE BULLETS WATUA SALAMA

Leo asubuhi timu ya Kenya Police Bullets FC imewasili salama mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mechi za ukanda wa Mataifa ya Afrika mashiriki kwa Wanawake CECAFA kuwania kufuzu kwa fainali za klabu bingwa afrika CAF itakayochezwa kuanzia Agosti 17 hadi Septemba 4, 2024.
Kocha mkuu Beldine Odemba alisafiri na kikosi cha wachezaji 24 kilichojumuisha wachezaji wapya waliosajiliwa akiwemo kipa wa Harambee Starlets Annedy Kundu, na mabeki Elizabeth Ochaka, pia nahodha wa Harambee Starlets na Norah Anne kutoka Vihiga Queens.
Wengine ni viungo Jane Hato kutoka timu ya wanawake ya Mathare United na Christine Nafula, na washambuliaji Bertha Omita na Emily Moranga kutoka Vihiga Queens.
Timu tisa zitachuana katika awamu ya kufuzu. Bullets ikipangwa Kundi ‘A’ pamoja na CBE (Ethiopia), Yei Joint FC (Sudan Kusini), Rayon Sport Women (Rwanda), na washiriki wa kwanza Warriors Queens (Zanzibar).
Timu moja pekee kutoka kanda ya CECAFA itafuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF inayopangwa baadaye mwaka huu.
Imetayarishwa na Nelson Andati