USIBAKI TU ODM, WAJACKOYA AMSHAURI ODINGA.
Huku kinara wa ODM Raila Odinga akiendeleza vikao vya mashauriano kabla ya kutoa mwelekeo wake wa kisiasa atakaochukua, kinara huyo sasa ametakiwa kutofanya mashauriano na wanachama wa ODM pekee na badala yake awashirikishe wakenya wote.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini, kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoya, amemtaka Odinga kufanya mashauriano na viongozi wengine wa vyama, huku akimwonya dhidi ya kufanya maamuzi ya haraka.
Wakati uo huo, ameitaka serikali kufutilia mbali miradi ya umma inayokabiliwa na pingamizi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































