MFAGIZI WA MAGEREZA AHUSISHWA NA UFUJAJI WA SH.450

Mhudumu wa usafi katika idara ya magereza kwa jina Eric Kipkururi Mutai, naibu kamishna mkuu na maafisa wengine wakuu kwenye idara hiyo ni miongoni mwa watu 13 wanaochunguzwa na tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kuhusiana na ufujaji wa shilingi milioni 450.
Kulingana na afisa wa EACC ambaye hajataka kujulikana kwani hana mamlaka ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, maafisa watano katika wizara ya usalama wa nchi wamekamatwa huku uchunguzi ukiendelea.
EACC imesema mhudumu huyo wa usafi anamiliki kampuni 7 ambazo zilizipokea shilingi milioni 250 bila kusambaza chochote kwa idara ya magereza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa