MKUTANO WA RAIS NA BARAZA JIPYA.
Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua wamefanya kikao na mawaziri na makatibu wakuu katika Ikulu ya Nairobi, siku chache baada ya kubuniwa kwa baraza jipya la mawaziri.
Wakati wa kikao hicho, Ruto amewaagiza viongozi hao kujiepusha na ufisadi na badala yake kuweka mbele mipango itayobuni nafasi za ajira kwa wakenya.
Aidha, amekariri kuwa lengo la kuwashirikisha viongozi wa upinzani serikalini ni kuliunganisha taifa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































