ONYONKA: RAILA ANAFAA KUTANGAZA MSIMAMO WAKE KUHUSU SWALA LA UTEKAJI NYARA WA WAKENYA

Seneta wa Kisii Richard Onyonka amemtaka aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kutangaza msimamo wake kuhusu visa vya utekaji nyara wa hivi majuzi vinavyolenga hasa vijana walioshiriki maandamano dhidi ya serikali.
Seneta huyo ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara na kuwataka walio karibu na Rais William Ruto kumshirikisha kuhusu suala hilo.
Onyonka aidha amebainisha kuwa taasisi za kidini kama pia zinapaswa kufanya kikao na rais kuhusu suala hilo muhimu.
Imetayarishwa na Janice Marete