SENETA MAALUM WA LAMU AITAKA SERKALI KUHARAKISHA UKARABATI WA MIUNDO MBINU LAMU

Seneta maalum katika kaunti ya Lamu Shakila Abdala ameitaka serikali ya kitaifa kupitia wizara ya barabara na uchukuzi nchini kutoa maelezo ya kina kuhusu miakakati ya kukarabati barabara ya Gamba katika kaunti ya Lamu na Tana River.
Kwa mujibu wa Shakila licha ya shughuli za usafiri kutatizika kila mwaka kutokana na mafuriko hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa kutatua changamoto hiyo.
Shakila vile vile ametoa wito kwa viongozi katika bunge la kitaifa Pamoja na wenzao wa kaunti ya Lamu na tana river kujitokeza na kutoa misaada mbali mbali kutumia fedha za hazina ya majanga zilizotengewa maeneo bunge yao.
Imetayarishwa na Janice Marete