DCI KUCHUNGUZA MADAI YA SIMU YA TALAM KUTUMIKA
Idara ya Dci imeagizwa kuchunguza madai ya kutumika kwa simu ya Ocs wa kituo cha central kutuma jumbe za kuitisha fedha kutoka kwa watu tofauti.
Hakimu mkuu katika mahakama ya milimani Benmark Ekhubi ameutaka upande wa mawakili wake Samson Talam kutotumia suala hilo kutia doa kwenye uchunguzi unaoendeshwa na mamlaka ya Ipoa.
Simu yake Talam ilichukuliwa na maafisa wa uchunguzi wa mamlaka hiyo kwa ukaguzi katika uchunguzi unaoendelea katika kifo tata cha mwalimu Albert Ojwang.
Imetayrishwa na Antony Nyonesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































