WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO LA MARIKITI WAANDAMANA KUPINGA KUFUKUZWA KATIKA SOKO HILO

Shughuli za biashana na usafiri zimetatizika katika barabara ya jogoo road na Haile Selasie Avenue baada ya wafanyibiashara wanaofanya biashara katika soko la Wakulima, maarufu Marikiti, kuandamana mapema leo wakiapa kusitisha shughuli zao hadi pale serikali ya kaunti itakapoondoa notisi ya kuwafurusha katika soko hilo.
Kulingana na wafanyabiashara hao, maafisa wa Baraza la Kaunti walifika katika eneo hilo wakiwataka waondoke katika soko hilo na kuamia katika soko la Kangundo Road.
Michael Wachira, ambaye ni mfanyibiashara, anasema kuwa soko la Kangundo Road tayari lina wafanyibiashara wengine na kwamba kuwafurusha kutawakosesha kazi.
Imetayarishwa na Janice Marete