#Football #Sports

FKF YAOMBWA KUHARAKISHA UJENZI WA VIWANJA

Serikali na Shirikisho la Soka la Kenya wamehimizwa kuharakisha ujenzi wa viwanja vya soka vya hadhi ya kimataifa na vilivyoidhinishwa na FIFA, ili kusaidia kukuza vipaji na kuandaa mechi za kimataifa.

Hii ni baada ya timu ya taifa ya soka ya wanawake U17, Junior Starlets, kuweka historia kwa kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA U17 litakaloandaliwa Jamhuri ya Dominika.

Kocha mkuu wa Kampi ya Moto United Academy ya Nakuru Robert Orangi Arasa alisema ni aibu kwa Starlets kuandaa mechi zao nchini Malawi, kutokana na ukosefu wa viwanja vilivyoidhinishwa na FIFA nchini Kenya.

Orangi pia alitoa wito kwa FKF kuhakikisha vijana hao wanalelewa vyema hata baada ya Kombe la Dunia.

Kocha huyo pia alionyesha matumaini kwamba timu ya taifa ya U17 itauteka ulimwengu huko Jamhuri ya Dominika.

Junior Starlets ilifuzu kwa Kombe la Dunia, baada ya kuishinda Burundi kwa jumla ya mabao 5-0, na kuwa timu ya kwanza ya kandanda ya Kenya kufuzu kwa michuano ya ulimwengu chini ya mwavuli wa FIFA.

Imetayarishwa na Nelson Andati

FKF YAOMBWA KUHARAKISHA UJENZI WA VIWANJA

NI NAFASI YA CHIPUKIZI WA STARLETS KUNG’AA

FKF YAOMBWA KUHARAKISHA UJENZI WA VIWANJA

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HIV YAPUNGUA KENYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *