MAGEUZI YATOKOTA, AZIMIO YATANGAZA
Mageuzi yanatarajiwa katika ulingo wa kisiasa nchini hivi karibuni baada ya kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa DAPK Eugene wamalwa kutangaza kujiondoa kwenye muungano wa Azimio na kubuni muungano tofauti wa upinzani kabla ya mwaka ujao.
Kulingana nao, huenda Musyoka akawa kinara wa muungano huo, na kuongeza kuwa lengo lao ni kutoa uongozi mbadala nchini.
Aidha, wamehimiza mshikamano miongoni mwa wanachama wa Azimio.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































