STRATHMORE BLADES WAONYESHA MAKALI YAO

Timu Ya Wanaume Ya Strathmore Blades Ilianza Vyema Mchujo Wa Ligi Kuu Ya Kitaifa Ya Mpira Wa Kikapu Nchini Kwa Kuwapepeta USIU Tigers 82-51 Katika Mchezo Wa Ufunguzi Wa Mechi Yao Ya Robo Fainali Iliyochezwa Katika Uwanja Wa Nyayo.
Blades Walikuwa Na Nguvu Katika Robo Zote, Wakipata Uongozi Mwembamba Wa 16-12 Baada Ya Robo Ya Kwanza Kabla Ya Kuweka Mwanya Wa 32-23 Wakati Wa Mapumziko.
Strathmore Haikuwahi Kuonyesha Dalili Za Kulegea Waliposogeza Alama Hadi 67-35 Katika Robo Ya Tatu Kabla Ya Kumaliza Kwa Kishindo 82-51.
Matokeo Mengine Ya Wikendi;
Equity Dumas 72-63 Ulinzi Warriors (Game 1)
Uon Terror 56-81 Thunder (Game 2)
USIU Flames 65-44 Strathmore Swords (W)
Zetech Sparks 77-26 Storms (W) (Game 1)
ANU 37-76 KPA (W) (Game 2)
KPA 79 ANU 53 (M) (Game 2)