#Sports

MICHEZO KAKAMEGA ZAENDELEA BAADA YA KUSITISHWA

Mashindano ya kandanda ya wavulana ya kanda ya Magharibi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa muda kufuatia rufaa ya Musingu High, kupinga uamuzi uliowaondoa kwenye kinyang’anyiro hicho sasa yataendelea kufuatia kukamilika kwa suala hilo leo jioni.

Ilibainika kwamba Musingu ilichezesha wachezaji wawili wasiostahiki – Boaz Muchiri na Harrison Amalemba dhidi ya mabingwa wapya wa Kaunti ya Kakamega Butere Boys katika fainali.

Hata hivyo, mahakama ya rufaa ya Kaunti ya Kakamega iliamuru mechi ya marudiano kati ya Musingu na Kakamega High, kwani Kakamega ilichapwa na Musingu kwenye nusu fainali – huku wachezaji wawili wasiostahiki wakishiriki.

Agizo hilo ambalo ni maafikiano ya wazi ya sheria zinazoweka wazi kufukuzwa kwa timu yoyote inayowachezesha wachezaji wasiostahiki, lilifanya mechi bado iendelee jioni ya leo, ili kubaini timu itakayoungana na Butere kuwakilisha Kaunti ya Kakamega katika ngazi ya ukanda.

.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MICHEZO KAKAMEGA ZAENDELEA BAADA YA KUSITISHWA

DILI YA MBEUMO YAACHELEWA KUIVA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *