MAHAKAMA YA UPEO YAFUTILIA USHINDI WA HARRISON GARAMA KOMBE
Mahakama ya upeo imedumisha uamuzi wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa wa kufutilia mbali ushindi wa mbunge wa magarnini Harrison Garama Kombe
Kombe alichaguliwa kupitia tiketi ya chama cha ODM alimshinda mpinzani wake wa karibu kwa kura 21 pekee.
Jopo la majaji watano wa mahakama limeamua kwamba mlalamishi Stanley Kinga Karisa alidhibitisha madai yake katika kesi hiyo kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa wakati wa ujchaguzi.
Kwa mujibu wa majai hao katiba haikufuatwa na kwamba kujlikuwa na ukiukaji wa sheria.
Kinga aliyekuwa spika wa bun ge la kaunti ya Kilifi aligombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha UDA ambapo alijizolea kura elfu 11925 dhidi ya Garama Kombe ambaye sasa ushindi wake umefutilkiwa mbali.
Imetayarishwa na Janice Marete.
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































