#Football #Sports

TUBORESHE UTENDEKAZI

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Murang’a Seal, Hussein Mohammed, ameitaka FIFA na Serikali ya Kenya kuunda Kamati ya Urekebishaji ili kusimamia utendakazi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).

Wito huu unafuatia amri ya hivi majuzi ya mahakama inayokataza uongozi wa sasa wa FKF kufanya shughuli zozote kwa niaba ya shirikisho, ikisubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo tarehe 7 Oktoba.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari mjini Karen – Nairobi, Mohammed alisema soka la Kenya liko katika hali mbaya, akihusisha hali hiyo na madai ya ukiukwaji wa sheria unaofanywa na uongozi wa sasa wa FKF.

Hussein pia ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kuchukua hatua haraka kulingana na mapendekezo kutoka kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu uwezekano wa ufujaji wa pesa na FKF.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TUBORESHE UTENDEKAZI

LIPO TUMAINI

TUBORESHE UTENDEKAZI

BUSIA YANAWIRI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *