#Football #Sports

VIDOSHO WA STARLETS WAWASILI UTURUKI

Harambee Starlets ikiongozwa na kocha Beldine Odemba imewasili salama nchini uturuki kushiriki michuano ya mualiko kuwania kombe la Pink Ladies kuanzia leo hadi tarehe 31 ya mwezi huu katika jiji la Antalya.

Kenya itaanza mchuano wao kwa mechi dhidi ya Chinese Taipei hapo kesho, ikifuatiwa na Urusi Jumamosi, Oktoba 26, na kuhitimisha dhidi ya Ufilipino Jumatano, Oktoba 30.

Haya ni mashindano ya kwanza ya kimataifa kwa timu hiyo mwaka huu, ikiwa imecheza mara ya mwisho katika mchujo wa WAFCON dhidi ya Botswana mnamo Desemba 5, 2023. Kenya ilikosa nafasi ya kutamba katika michuano ya bara baada ya kushindwa na Botswana kwa jumla ya mabao 2-1. Walitoka sare ya 1-1 nyumbani kabla ya kufungwa 1-0 mjini Gaborone.

Kikosi kilichotajwa na kocha Beldine kwa kiasi kikubwa kina wachezaji wa ligi za ndani, huku wachezaji wa kigeni kama Vivian Nasaka, nahodha Ruth Ingosi, na Wincate Kaari wakijumuishwa.

Baadhi ya wachezaji wa kawaida kikosini humo kama Corazon Aquino, Jentrix Shikangwa, Mwanahalima Jereko, Carolyn Rufa, Esse Akida, Terry Engesha miongoni mwa wengine wameachwa nje ya kikosi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

VIDOSHO WA STARLETS WAWASILI UTURUKI

WATAKAOUTUZWA WACHAGULIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *