#Local News

UOKOAJI WAENDELEA KWENYE MGODI KAKAMEGA

Familia za waathiriwa waliokwama kwenye vifusi baada ya kuangukiwa na ukuta wa mgodi wa dhahabu katika eneo la Shinyalu kaunti ya Kakamega zimehakikishiwa kuwa shughuli za uokoaji zitaendelea hadi wapendwa wao watakapookolewa.

Zoezi la uokoaji linaongozwa na maafisa wa usalama kwenye kaunti hiyo, wachimbaji migodi 12 wakihofiwa kukwama ndani ya mgodi huo.

Jumla ya wachimba migodi 20 walikuwa kwenye eneo hilo wakati wa mkasa huo wa jana jioni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *