MAGEUZI MAPYA SEKTA YA CHAI YAJADILIWA
Wakulima wa chai nchini huenda wakapata afueni kufuatia mikakati mipya ya mageuzi iliyoandaliwa na Wizara ya Kilimo huku Katibu wa wizara hiyo Kiprono Ronoh akikutana na wadau wa sekta ya chai kujadili namna ya kuongeza uzalishaji, kupanua masoko na kuboresha kipato cha mkulima.
Wadau wamesisitiza umuhimu wa utafiti wa kina ili kuinua ubora wa chai na kuifanya ikubalike zaidi kwenye soko la kimataifa. Pia wamependekeza matumizi ya teknolojia na usimamizi bora ili kuhakikisha wakulima wananufaika zaidi kutokana na jasho lao.
Mageuzi hayo yanalenga kuwaweka wakulima wa Kenya katika nafasi bora zaidi kimataifa na kuinua maisha yao.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































