GACHAGUA KIZIMBANI?

Mwanaharakati kwa jina Frederick Bikeri amemshtaki Naibu Rais Rigathi gachagua mahakamani kuhusiana na matamshi ya Gachagua dhidi ya mkurugenzi wa idara ya ujasusi NIS Noordin Haji.
Kulingana na mwanaharakati huyo, matamshi ya Gachagua dhidi ya Haji hayana ukweli, yenye uchochezi na kinyume na sheria, na kwamba hayaambatani na viwango vya mienendo ya mtumishi wa umma kulingana na vipengee vya 73 na 75 vya katiba pampoja na sheria ya maadili
Kupitia wakili Danstan Omari, bikeri anasisitiza kwamba tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC inafaa kumchunguza matamshi ya Gachagua anayosema yalilenga kuzidhalilisha afisi za mkurugenzi wa mashtaka ya umma na ile ile ya ujasusi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa