WANAFUNZI TURKANA WAANDAMANA KUPINGA UHAMISHO WA MWALIMU
Wanafunzi wa shule ya mseto ya upili ya Kalobeyei eneo la Kakuma kaunti ya Turkana wameandamana na kutembea kwa umbali wa kilomita 30 hadi katika afisi ya mkurugenzi wa elimu eneo hilo wakilalamikia hatua ya tume ya TSC kumhamisha mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, mwalimu aliyehamishwa amekuwa akichangia matokeo bora kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita.
Wakati wa maandamano hayo, imewalazimu maafisa wa usalama wakiongozwa na OCS wa Kakuma Vincent Ekamais na wakuu wa elimu kuwakuta barabarani ili kuwatuliza.
Hata hivyo, wameapa kwamba hawatarudi shuleni hadi mwalimu huyo arejeshwe, huku mkuu wa elimu eneo hilo Henry Lubanga akiahidi kufanya kikao na bodi ya shule.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































