MSHUKIWA MAHAKAMANI KWA ‘KUMNAJISI’ MTOTO BUSIA
Polisi katika kaunti ya Busia wanatarajiwa kumfikisha mahakamani hii leo mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 44, aliyekamatwa kwa madai ya kumnajisi mpwa wake msichana mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Nabutuki eneo bunge la Funyula.
Kulingana na OCPD wa Samia Richard Moracha, msichana huyo alifichua unyama aliotendewa na mjomba wake na kusababisha kukamatwa kwa mshukiwa ambaye amekesha katika kituo cha polisi cha Sio Port.
Anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Port Victoria ambayo maajuzi ilimpa hukumu ya miaka 25 mwanamme mwingine kosa la kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 14.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































