#Business

MAKADIRIO YA BAJETI YA 2025-26

Serikali kuu imewasilisha bajeti ya shilingi trilioni 4.2 (kiwango sawa na dola bilioni 32.5 za Marekani) kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026, ikiwa na mapendekezo yanayolenga kuchochea shughuli za kiuchumi.

Waziri wa fedha na mipango ya uchumi nchini John Mbadi, amewasilisha taarifa ya bajeti mbele ya Bunge la taifa, na kusema serikali inataka kuhimiza ukuaji endelevu wa uchumi ili kuboresha maisha ya watu, kuchochea biashara na ustawi wa viwanda.

Hata hivyo, Mbadi amesema mwaka 2024, uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 4.7, ukichochewa na ukuaji chanya katika sekta zote isipokuwa ujenzi na madini, na kuwa wa chini ikilinganishwa na asilimia 5.7 ya mwaka 2023, hasa kutokana na athari za mafuriko katika robo ya pili na maandamano ya kupinga sheria ya fedha katika robo ya tatu ya mwaka 2024.

Licha ya kudorora huko Mbadi amesema uchumi wa Kenya unaendelea kuwa thabiti, na kurekodi kiwango cha wastani cha ukuaji wa asilimia 5.2 kwa mwaka 2023 na 2024, na kupita ukuaji wa kimataifa wa asilimia 3.3, na asilimia 3.8 ya eneo la kusini mwa Sahara.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

MAKADIRIO YA BAJETI YA 2025-26

CHANJO ZAWASILI NCHINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *