#Local News

AFUENI KWA JAJI KULLOW

Jaji wa mahakama ya ardhi na mazingira aliyesimamishwa kazi Mohammed Kullow amepata afueni baada ya jopokazi lililobuniwa na Rais William Ruto kumwondolea tuhuma za utovu wa nidhamu, kushindwa na kazi na ukiukaji wa sheria za idara ya huduma za mahakama zilizokuwa zikimwandama.

Baada ya uchunguzi kwa takribani mwaka mmoja, jopokazi hilo likiongozwa na jaji Patrick Kiage limesema baada ya kutathmini Ushahidi uliowasilishwa, limekosa kumpata na hatia na hivyo kupendekeza kwamba Rais Ruto amrejeshe kazini.

Rais Ruto alibuni jopokazi hilo mnamo Machi mwaka jana baada ya idara ya huduma za mahakama kuwasilisha malalamishi dhidi yake kwa rais.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AFUENI KWA JAJI KULLOW

KOECH: WAZIRI MUTURI ATAONDOLEWA MAMLAKANI

AFUENI KWA JAJI KULLOW

JUHUDI ZA KUBORESHA AFYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *