AMIN ATARAJIWA KUMWASILISHA NDIANGUI MAHAKAMANI
Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI Mohammed Amin anatarajiwa kuviongoza vitengo vya usalama kumwasilisha mahakamani bloga Ndiangui Kinyagia mahakamani katika hali yoyote ile, baada ya mahakama kumwagiza Amin amfikishe bloga huyo mahakamani hii leo.
Kwenye uamuzi wake Jumanne wiki hii, jaji Chacha Mwita alimwagiza Amin amfikishe Kinyangia mahakamani au mwili wake kabla ya kesi kuendelea, licha ya Amin kupitia kwa mawakili wake kukana kuwa na ufahamu kuhusu bloga huyo aliyetoweka takribani wiki 2 zilizopita.
Kulingana na jaji Mwita, maafisa wa DCI ndio wanaopaswa kuwajibishwa kwenye tukio hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































