LAWAMA ZA UONGOZI UON

Utata wa uongozi wa chuo kikuu cha Nairobi sasa umechukua mkondo tofauti, viongozi wa wanafunzi chuoni humo wakimlaumu waziri wa elimu Julius Ogamba kwa madai ya kuhitilafiana na uongozi wa chuo hicho.
Haya yamejiri baada ya Ogamba kuwahamisha wanachama 4 wa baraza la usimamizi wa chuo hicho hadi katika vyuo vikuu vingine 3 ambavyo ni Karatina, Mama Ngina Embu na University of Eldoret.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa