VIONGOZI WA ODM KAKAMEGA WAMFOKEA JUSTUS KIZITO KWA KUDAI KUWA KIONGOZI WA CHAMA HICHO

Viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Kakamega wamejitokeza kupinga madai aliyoibua aliyekuwa mbunge wa Shinyalu Justus Kizito kwamba ndiye mwenyekiti halali wa chama cha ODM kaunti ya Kakamega.
Viongozi hao wanasema kuwa Kizito hana mamlaka ya kujihusisha na maswala ya uongozi wa chama hicho kwa kuwa alikigura alipokuwa akitafuta kiti cha ubunge wa Shinyalu 2022 na kwamba gavana Fernandez Barasa ndiye wanayemtambua kama mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kakamega.
Imetayarishwa na Janice Marete