#Football #Sports

ULINZI STARLETS WAKO TAYARI KWA MICHEZO YA FKF

Miamba wa soka la akina dada nchini Kenya Ulinzi Starlets wamekamilisha maandalizi yao kulekea fainali ya kombe la FKF itakayosakatwa hii leo adhuhuri ugani Police Sacco Nairobi wakiongozwa na kocha mkuu Joseph wambua Mwanza aliyeeleza imani ya kunyakua taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Ulinzi walifuzu fainali hiyo kwa kuwabandua mabingwa wapya wa ligi kuu FKF Kenya Police Bullets kwa mabao 4-2 ya penanti ugani Dandora mnamo Mei tarehe 4 wakati wapinzani wao Kibera wakiwatoa Zetech Sparks 2-1 kwenye nusu fainali nyingine.

David Vijago ni kocha wa Kibera anayesema wamejipanga vyema kwa fainali hiyo.

Fainali hiyo iliyohairishwa mara tatu itatanguliwa na mchezo wa saa tano asubuhi wa kumsaka mshindi wa tatu kati ya Zetech Sparks na Kenya Police Bullets.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ULINZI STARLETS WAKO TAYARI KWA MICHEZO YA FKF

KARUA ATOFAUTIANA NA RUTO, RAILA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *