WAPE MTIHANI KAMA WAKO SAWA, OGAMBA

Huku masomo ya vyuo vikuu yakiendelea kuathirika kutokana na mgomo wa wahadhiri, waziri wa elimu Julius Ogamba amewataka wasimamizi wa vyuo hivyo kuwapa wanafunzi mitihani ya mwisho wa muhula iwapo wana uhakika kwamba wanafunzi wamepokea mafunzo ya kutosha.
Akizungumza mapema leo baada ya uzinduzi wa usambazaji wa karatasi za mtihani wa KCSE katika kaunti ya Nyamira, Ogamba amesema wizara yake inasaka suluhu ya kudumu kwa migomo ya mara kwa mara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa