#Local News

MGOMO WA MAKANGA KITALE

Kwa siku ya pili sasa kituo kikuu cha magari mjini kitale kimesalia bila magari na kulazimika kuhudumu nje ya stegi hali ikichangia kutatizika kwa huduma za usafiri na uchukuzi kwa magari yanayo hudumu kutoka kitale hadi jijini Nairobi na maeneo mengine

Naibu mwenyekiti wa makanga katika kaunti hiyo Mike Ochola amesema hatua hiyo imechukuliwa kulalamikia usimamizi mbaya wa uongozi wa makanga katika kituo cha magari hadi wakati amabapo gavana wa kaunti hiyo George Natembea atakapofanya kikao maalum nao na kulainisha mambo

Kwa mujibu wa ochola shughuli za utozaji kodi zimetatizika na kwamba sharti uchaguzi mpya ufanywe ili mambo yawekwe wazi na uongozi mpya utakaochaguliwa

Imetayarishwa na: Janice Marete

MGOMO WA MAKANGA KITALE

MAHAMAKA YA MAVOKO IMECHOMEKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *