WAKAZI MUMIAS WAMTETEA SALASYA

Wakazi wa eneo la Mumias Mashariki wamejitokeza kukosoa hatua ya mbunge wao Peter Salasya kufurushwa na hata kujeruhiwa na kundi la mashabiki na wahuni kutoka uwanja wa michezo wa Nyayo jijini Nairobi siku 2 zilizopita, wakikariri kuwa mbunge huyo ana haki ya kujieleza kama kiongozi aliyechanguliwa.
Wakizungumza na wanahabari, wakazi hao wamesema hawataruhusu kiongozi wao kudhalilishwa, wakihusisha tukio hilo na ukosoaji wake wa baadhi ya viongizi wa kisiasa nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa