JUHUDI ZA MASKAUTI KUIMARISHA LISHE POKOT

Katika juhudi za kuimarisha masomo kwa kupunguza muda unaopotezwa wakati wa kusaka chakula cha mchana, chama cha maskauti katika kaunti ya Pokot Magharibi kimeanzisha mafunzo kwa wanafunzi na baadhi ya shule kuhusu umuhimu wa kukuza vyakula shuleni.
Kulingana na chama hicho, hatua hiyo itawawezesha wanafunzi kutumia muda huo kusoma na hivyo kuboresha masomo yao.
Kaunti hiyo ni mojawapo ya kaunti ambazo viwango vya masomo huathirika na ukame wa chakula.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa