#Local News

MGOMO WA UASU WAZIMWA, MAHAKAMA YAAGIZA MAZUNGUMZO

Ni afueni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu baada ya mahakama ya uajiri na leba kusitisha mgomo wa wafanyakazi wa vyuo vikuu vya umma ambao umeanza hii leo kupitia muungano wa UASU.

Jaji wa mahakama hiyo Jacob gakeri, ametoa agizo hilo baada ya mabaraza ya vyuo vikuu na shirikisho la uajiri nchini FKEkuwasilisha kesi mahakamani.

Aidha, jaji Gakeri ameorodhesha kesi hiyo kuwa ya dharura, na kuwahimiza wahusika wafanye mazungumzo ili kupata suluhu.

Wafanyazi hao wameanza mgomo wao leo baada ya makataa yao ya siku 7 kukamilika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MGOMO WA UASU WAZIMWA, MAHAKAMA YAAGIZA MAZUNGUMZO

RUTO AAGIZA UPATANISHI KWA MAHAKAMA, POLISI

MGOMO WA UASU WAZIMWA, MAHAKAMA YAAGIZA MAZUNGUMZO

BUNGE LAMWIDHINISHA KANJA KUWA INSPEKTA MKUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *