PS KIMUTAI: UNICEF KUSAMBAZA CHANJO ZAIDI

Katibu mkuu katika wizara ya fedha Harry Kimutai amesema wizara hiyo imetenga shilingi bilioni 1.25 zitakazotumika kwa ununuzi wa chanjo za watoto kufuatia upungufu wa chanjo hizo hapa nchini.
Katika taarifa, Kimutai aidha mesema serikali inaendelea na mzungumzo na shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF kuharakisha katika usambazaji wa dawa hizo.
Chanjo za Polio, BCG na ukambi ndizo zimeshuhudia upungufu nchini kutokana na deni kubwa ambalo seriklai inadaiwa na mashirika yanayosambaza chanjo hizo.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa