CHRISTIANO AMETAJWA KWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA URENO
Cristiano dos Santos, mtoto mkubwa wa mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or Cristiano Ronaldo, ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno cha Vijana wasiozidi umri wa miaka 15.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 14, ambaye kama babake anachezea Al-Nassr ya Saudi Arabia, pia amewahi kuwa na vilabu vya zamani vya Ronaldo vya Manchester United na Juventus.
Vijana wa Selecao walio chini ya umri wa miaka 15 watamenyana na Japan, Ugiriki na England katika dimba la Vlatko Markovic la vijana huko Croatia kati ya Mei 13-18.
Ronaldo, mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid na bado ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno akiwa na umri wa miaka 40, ana watoto watano.
Mshambuliaji huyo alishinda Euro 2016 akiwa na taifa lake, na kuisaidia kunyanyua taji lao la kwanza kuu, ingawa alitoka akiwa ameumia mapema kwenye fainali hiyo dhidi ya Ufaransa.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































