MICHEZO YA SHULE ZA UPILI ZIMESHIKA KASI

Michezo ya shule za sekondari muhula wa pili, ambayo inajumuisha Raga ya wachezaji saba (Rugby 7’s),
kandanda, mpira wa vikapu 3×3, voliboli, mpira wa pete (netball) miongoni mwa mingine,
imeng’oa nanga katika ngazi za kanda katika maeneo mbalimbali nchini.
Kocha mkuu wa mabingwa wa zamani wa raga ya wachezaji saba ya Koyonzo Boys, Eliud
Okwemba, ametaja kuwa ana matumaini kuwa timu hiyo itatwaa taji la ushindi kwa mara ya
tatu hasa ikihusishwa kwamba michezo ya kitaifa na ile ya Afrika Mashariki itafanyika kwao
nyumbani, Kakamega.
Koyonzo, wanatarajiwa kuhusika katika mashindano ya Scrummage yatakayofanyika huko
Kakamega ili kupima uwezo wao kabla ya michezo ya kitaifa.
Imetayarishwa na Nelson Andati