MAHAKAMA YASITISHA UCHAGUZI WA KJSA
Mahakama kuu imesitisha kwa muda uchaguzi wa wanachama wa baraza la kitaifa la muungano wa wafanyakazi wa idara ya mahakama KJSA uliopangiwa kufanyika jumamosi.
Uamuzi huo umetolewa baada ya wafanyakazi watatu wa idara ya mahakama kuelekea mahakamani kupinga uchaguzi huo.
Vincent Gikunda, Oscar Soi Anthony Oniala na Frank Megiri waliwasilisha maombi ya kuwania nyadhifa katika baraza hilo kabla ya kukosa kujumuishwa kuwa miongoni mwa wawaniaji.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































