MECHI YA REAL MADRID YAHAIRISHWA KUFATIA MAFURIKO
Mechi ya Real Madrid ya ugenini dhidi ya Valencia katika La Liga wikendi hii iliahirishwa siku ya Alhamisi na shirikisho la soka la Uhispania kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 95.
Mechi ya Villarreal ya nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano pia ilisitishwa baada ya mafuriko makubwa yaliyotokea mashariki mwa Uhispania.
La Liga iliomba shirikisho la soka la Uhispania (RFEF) kuahirisha mechi za Valencia na Villarreal siku ya Jumamosi, pamoja na michezo mitatu ya ligi daraja la pili inayohusisha timu kutoka maeneo yaliyoathirika.
Shirikisho hilo lilikuwa tayari limeahirisha mechi kadhaa za raundi ya kwanza ya Copa del Rey katikati ya wiki ukiwemo mchezo wa Valencia dhidi ya Parla Escuela.
Kipindi cha ukimya kwa wahasiriwa wa mafuriko kitafanyika kwenye mechi wikendi hii nchini Uhispania, ikijumuisha viongozi wa ligi Barcelona derby ya Kikatalani dhidi ya Espanyol siku ya Jumapili.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































