LSK YATAKA AFISA ALIYEKUWA NA ‘MUUAJI’ AKAMATWE
Chama cha wanasheria nchini LSK kinashinikiza kukamatwa kwa afisa wa polisi aliyekuwa Pamoja na afisa anayesemaekana kukamatwa baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya mchuuzi katikati mwa jiji la Nairobi hapo jana.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, rais wa LSK Faith Odhiambo, amesisitiza kuwa wawili hao walikuwa wakishirikiana, na hivyo wote wanafaa kukamatwa na kushtakiwa.
Aidha, ameitaka mamlaka ya IPOA kutoa ripoti yake kuhusu hatua ilizochukua kwenye uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































