KQ YAPATA FAIDA YA DOLA MILIONI 41.7

Licha ya changamoto katika sekta ya usafiri wa anga, Kenya Airways (KQ) imepata faida ya dola milioni 41.7 katika mwaka wa fedha 2024, ikitoka kwenye hasara ya dola milioni 174.6 mwaka 2023.
Mkurugenzi Mkuu, Allan Kilavuka, amesema mafanikio haya yanaashiria mabadiliko makubwa, huku shirika likiendelea kuwavutia wawekezaji wa kimkakati.
Mwenyekiti wa KQ, Michael Joseph, amesema matokeo haya yameweka rekodi mpya kwa idadi ya abiria na mapato, yakionyesha ukuaji wa shirika hilo.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi