#Local News

POLISI WACHUNGUZA MAUAJI HUKO MALAVA

Polisi wameanzisha uchunguzi wa mauaji ya mzee wa miaka 73 katika kijiji cha Ikoli, Malava, huku Mkewe akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitalini.

Inadaiwa washambuliaji walivamia boma lao usiku wa manane, wakimuua mzee huyo na kumkata ulimi mkewe huku ripoti za awali zinaonyesha kuwa marehemu alikataa kutoa hati ya ardhi kwa ndugu zake.

Chifu Moses Namutali amewataka wakazi kuwa watulivu huku uchunguzi ukiendelea. Marehemu ameacha wake wanne na watoto 34.

Imetayarishwa na Janice Marete

POLISI WACHUNGUZA MAUAJI HUKO MALAVA

OILERS WATINGA FAINALI YA ESS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *