#Local News

MWANAHARAKATI BOB NJAGI AVUNJA UKIMYA BAADA YA KUTEKWA NYARA KWA SIKU 32

Mwanaharakati Bob Njagi, kiongozi wa chama cha Free Kenya Movement, hatimaye amezungumza kuhusu kutekwa nyara kwake kwa siku 32, kufuatia kuachiliwa kwake na watekaji nyara.

Katika mkutano na wanahabari wenye hisia kali uliofanyika mtaani Kitengela kaunti ya kajiado pamoja na wanaharakati wenzake, Njagi amesimulia tajriba ya kutisha aliyovumilia, ambayo anahusisha na jukumu lake katika maandamano ya gen-z dhidi ya serikali.

Njagi ameeleza jinsi alivyotekwa nyara Agosti 19 alipokuwa akisafiri kwa matatu huko Mlolongo kaunti ya Machakos Watu wanne waliojifunika nyuso zao walimkaribia, wakimtuhumu kubeba bunduki.

Njagi ameelezea hali mbaya ya utumwa wake, akisema alinyimwa chakula kwa siku mbili za kwanza na kulishwa mara mbili tu kwa wiki baadaye.

Watekaji nyara wake walimruhusu kuoga mara moja tu kwa juma, na hivyo kumwacha katika hali ya kukata tamaa ya kimwili na kihisia-moyo daima.

Licha ya masaibu hayo, Njagi amechagua kuwasamehe waliomteka, lakini bado ameazimia kuiwajibisha serikali kwa masaibu aliyopitia.

Njagi amefichua mipango yake ya kushtaki jimbo hilo, sio tu kwa kukiuka haki zake bali pia kukomesha visa vinavyoongezeka vya utekaji nyara kote nchini.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *